Michezo

Waziri Mwakyembe amepiga marufuku ‘Taifa’ kuitwa kwa ‘Mchina’

on

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dr Harrison Mwakyembe leo February 14 2019 alifanya mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kuzindua rasmi nembo itayotumika kama ishara za fainali za michuano mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 (AFCON-U17).

Katika uzinduzi huo Waziri Mwakyembe pia alitumia fursa hiyo kuwaonya watu na wadau wa soka ambao hawajivunii kuwa na uwanja wa Taifa kwa kuliita jina hilo, badala yake wameanza kukuza jina la kuitwa kwa “Mchina” Waziri alisema ni bora uitwe hata kwa Rais Mkapa sababu ulijengwa chini yake.

“Hebu tuwe waangalifu kidogo kwenye kuanzisha misemo na vibwagizo kwenye michezo ambavyo vinaweza kupotosha na visisaidie sana kujenga utaifa, kwa mfano imejitokeza fashion sasa ya kuita uwanja wa Taifa kwa Mchina, mimi naomba tu niseme wazi huu ni upuuzi uliopitiliza, naomba msiite uwanja huu kwa mchina, uwanja huu hatukupewa zawadi na mchina ulitokana na kodi ya mtanzania”>>> DR Mwakyembe

Imeshinda Simba SC tabu kaipata JB wakati wa kutoka

Soma na hizi

Tupia Comments