PremierBet Ad
Asas Dairies Ad
NBC Ad

Habari za Mastaa

Private Jet ya Davido imewasili tayari Nigeria

on

Staa Davido kutokea Nigeria anazidi kututhibitishia kuwa hela yake sio ya mchezo na hii ni baada ya kutuonyesha private jet yake kuwasili katika ardhi ya Lagos,Nigeria kupitia insta story yake na kuandika ujumbe wa kuthibitisha ujio wa ndege hiyo binafsi.

Kupitia Insta story ya Davido amepost ngazi za ndege hiyo na kuandika ujumbe unaosomeka “Tuko juu sasa hivi, ndio ndege yangu imeshawasili” ikiwa imeambatana na picha nyingine na kusema “Imefika”

Ikumbukwe tu May 11,2018 kupitia mtandao wa twitter Davido alitudokeza kuhusiana na ujio wa ndege hiyo binafsi na kusema kuwa itawasili hivi karibuni na itamsaidia katika ziara zake za muziki ndani na nje ya bara la Afrika.Ujio wa ndege hiyo ya Davido inamfanya kuwa miongoni mwa mastaa wachache wanaomiliki ndege binafsi duniani.

HISTORIA: Alivyopata jina Majuto | Kuacha Jeshi | Rekodi anayoshikilia | Umauti

Soma na hizi

Tupia Comments