Habari za Mastaa

Rappa Kendrick Lamar amekuwa msanii wa kwanza kupata tuzo hii

on

Rappa maarufu kutokea nchini Marekani Kendrick Lamar amekuwa msanii wa kwanza katika tasnia ya muziki wa Hip Hop kupokea tuzo ya Pulitzer ikiwa ni tuzo yenye ufahari mkubwa katika muziki wa Marekani

Rappa huyo ameshinda tuzo ya Pulitzer katika Album yake ya “Damn” ambayo alifanikiwa kuiachia April, 2017 na kuwa msanii wa kwanza kupata tuzo hiyo katika historia ya miaka 100 ya Pulitzer kutokea nje ya dunia ya muziki wa Jazz na Classic.

Mashairi ya muziki wa Jazz anayotunga Rappa Kendrick Lamar yamemfanya kuwa na ushawishi mkubwa wa muziki katika kizazi cha muziki hasa kwa upande wake.

Miaka iliyopita katika tuzo za Pulitzer walifanikiwa kushinda Wynton Marsalis na Ornette Coleman katika kipengele cha muziki wa Jazz.

Onyo alilotoa January Makamba kwa Mastaa wa Bongo

 

Soma na hizi

Tupia Comments