PremierBet Ad
Asas Dairies Ad
NBC Ad

Habari za Mastaa

D’Banj amaliza mazishi, awashukuru waliojitokeza

on

Staa maarufu kutokea Nigeria D’Banj ametoa shukrani zake za dhati kwa wale wote waliojitokeza na kukamilisha zoezi la kumpumzisha mwanae Daniel katika nyumba yake ya milele kupitia ukurasa wake wa instagram.

D’Banj alipata taarifa za kifo cha mwanae Daniel aliyekuwa na umri wa mwaka mmoja siku ya June 24,2018 akiwa nchini Marekani kwaajili ya tuzo za BET, kifo hicho kilisababishwa na kuzama kwenye swimming pool.

Kupitia ukurasa wa instagram wa D’Banj ameandika “Tunataka kutumia mtandao huu kutoa shukrani kwa kila mmoja ambaye alizidisha mkono wake katika kushirikiana na sisi katika kipindi hiki kigumu, kwa niaba yangu na familia tunashukuru kwa mapenzi yaliyotoka kwa ndugu wa mbali na karibu. Mungu awabariki”

Dj Vasley aliyepata mafanikio kupitia Davido kumtumia kwenye Show zake

Soma na hizi

Tupia Comments