Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

“ROMA aliitwa BASATA amepewa miezi 6, hatumuulizi” – Juliana Shonza

on

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza ameongea na waandishi wa Habari baada ya kutangaza kumfungia Msanii wa Bongofleva Pretty Kind kutojihusisha na masuala ya sanaa kwa miezi sita.

Akiongea na waandishi wa habari Shonza amegusia pia suala la msanii ROMA ambapo amesema BASATA walimuita na kumuagiza akafanye editing katika wimbo wake wa KIBAMIA.

“Tumemuita ROMA miezi 2 iliyopita tumempa miezi 6 aurekebishe wimbo wake KIBAMIA na alikiri kweli ameimba vitu ambayo ni matusi, sisi hatuwezi mfuatilia kama amefanya editing au hajafanya, asipofanyia editing hizi sheria zitamhusu,”– Juliana Shonza

VIDEO: “HATAKIWI KUIMBA, WALA KUPOST CHOCHOTE KATIKA MITANDAO KWA MIEZI 6”- JULIANA SHONZA

Soma na hizi

Tupia Comments