Michezo

Kejeli za mashabiki wa Atletico kwa Ronaldo nae amezijibu kwa kejeli

on

Usiku wa February 21 201i lichezwa game ya kwanza ya hatua ya 16 bora ya UEFA Champions League kati ya Atletico Madrid dhidi ya Juventus ya Italia, katika mchezo huo Juventus ikiwa na nyota wake wa kimataifa wa Ureno Cristiano Ronaldo walikuwa ugenini wakicheza game hiyo na Atletico katika jiji la Madrid.

Game hiyo ilimalizika kwa Atletico Madrid kupata ushindi wa 2-0 hivyo wana kazi ya kwenda Turin Italia kutafuta sare tu ili waingie robo fainali, wakati wa mchezo huo na baada mashabiki wa Atletico Madrid walikuwa wakimkosoa Ronaldo kwa kumwambia alipe kodi kama sehemu ya kejeli kwani Ronaldo alikuwa anakesi ya ukwepaji kodi nchini Hispania.

 

Wakati kejeli hizo zikiendelea Ronaldo nae aliwajibu kwa kejeli kuwa ametwaa Champions League mara tano wakati wao hawajawahi chochote, “Nimetwaa Champions League mara tano na hawa jamaa sifuri” Atletico watarudiana na Juventus March 12 2019.

Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera kataja walichozidiwa wachezaji wake na Simba

Soma na hizi

Tupia Comments