Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

Safari ya Mzee Majuto imeiva fahamu siku atakayokwenda

on

Chama Cha Waigizaji Kinondoni kimethibitisha kukamilika kwa Safari ya Mzee Majuto kuelekea nchini India kwenye Hospitali ya Apollo kwa matibabu huku akisindikizwa na Daktari wa Wizara na Wanafamilia wawili , Safari inayotarajiwa kufanyika siku ya ijumaa ya tarehe 04 May 2018 .

Safari hiyo ambayo imefanikishwa na serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kusimamiwa na Waziri wake Mwakyembe itafanyika siku ya Ijumaa muda ni saa 7 mchana hivyo chama cha waigizaji Kinondoni kinawaomba mashabiki wa mzee Majuto kujitokeza kwa wingi kumuaga.

Pamoja na hilo Chama hicho kimetoa shukrani za dhati na za kipekee kabisa kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli na Serikali yake yote hususan wizara ya Habari , Utamaduni , Sanaa na Michezo chini ya Waziri Harrison Mwakyembe na timu yake yote ya wizara kwa ushirikiano wao na waigizaji.

Mzee Majuto azidiwa, arudishwa tena Hospitali kwa tatizo jingine

UZALENDO KWANZA: Ni time ya Tanga, Steve Nyerere kaweka wazi yatakayofanyika

Soma na hizi

Tupia Comments