PremierBet Tanzania Usain Bonus Ad

Michezo

Mbao FC sio watu wazuri, Simba waziacha point tatu Mwanza

on

Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2018/2019 imeendelea tena leo kwa michezo mitatu kuchezwa, Bingwa mtetezi Simba SC leo ameshuka dimbani kucheza mchezo wake wa nne wa Ligi Kuu msimu huu dhidi ya Mbao FC katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.

Simba katika mchezo huo walishuka dimbani wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza point mbili katika mchezo wao wa mwisho waliocheza katika uwanja wa Nangwanda Sijaona dhidi ya Ndanda FC baada ya kutoka sare tasa.

Mbao FC wakiwa nyumbani wamefanikiwa kuiadhibu Simba SC kwa ushindi wa goli 1-0, goli ambalo lilifungwa mapema dakika ya 27 na Said Khamis kwa mkwaju wa penati, ushindi huo umewafanya Mbao wafikishe jumla ya point 10 na kuongoza Ligi wakati Simba wakiwa nafasi ya tano kwa kuwa na point saba.

EXCLUSIVE: Licha ya kuwa na pesa na ustaa, hii ndio Sababu inayomfanya Samatta asiringe

Soma na hizi

Tupia Comments