Michezo

Simba SC wapangwa na Waswaziland, Mtibwa watupwa Seychelles

on

Shirikisho la soka Afrika CAF leo limepanga ratiba ya michezo ya kwanza ya michuano ya CAF Champions League na michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, ambapo Tanzania tunawakilishwa na Simba na Mtibwa Sugar.

Simba itaiwakilisha Tanzania katika michuano ya CAF Champions League baada ya kuwa Mabingwa wa Tanzania msimu uliopita, wakati Mtibwa Sugar wao wataiwakilisha Tanzania katika michuano ya Kombe la Shikisho Afrika baada ya kutwaa Kombe la FA msimu uliopita.

Baada ya ratiba kupangwa Simba wamepangwa kucheza mchezo wa kwanza nyumbani kati ya November 27-28 2018 dhidi ya Mbabane Swallows ya Swaziland na marudiano December 4-5 2018, Mtibwa Sugar wao wamepangwa na Northern Dynamo ya Seychelles na marudiano December 4 au 5 2018.

Hakuna anayemkuta Samatta kwa sasa Jupiter Pro League 2018/19

Soma na hizi

Tupia Comments