Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Marehemu Stan Lee afunguliwa kesi ya unyanyasaji wa kingono

on

Kwa mujibu wa mtandao wa The Blast umeripoti kuwa mwandishi na mchapishaji wa vitabu Marehemu Stan Lee kutokea nchini Marekani amefunguliwa shitaka na mfanyakazi wake Maria Carballo na kudai kuwa aliwahi kumnyanyasa kingono.

Mwezi wa April,2018 Maria Carballo alidai kuwa Stan Lee alikuwa akimuita kwenye hoteli ya Regency iliyopo Chicago kwa ajili ya kumkanda mwili wake (massage)  lakini alionekana kuwa na lengo tofauti na kile ambacho aliitiwa kukifanya na kusisitiza kuwa alipokuwa akifanya kazi yake ya massage Lee alikuwa akitoa sauti za mahaba.

Mbali na hilo Maria Carballo alisisitiza kuwa Lee alikuwa akimfanyia hivyo na ilimlazimu kuacha massage na kuondoka katika hotel hiyo na kuchukia kiasi chake cha pesa ambacho kulipwa kwa kazi hiyo kilikuwa dola 240 za Kimarekani sawa na zaidi ya shilingi laki tano za Kitanzania.

Inaelezwa kuwa Stan Lee ambae alifariki November 12,2018 kesi yake ilionekana kusimamishwa huku jaji mkuu akiamuru kesi hiyo kutupiliwa mbali na kudaiwa kuwa Maria Carballo anataka fidia ya kiasi cha dola za Kimarekani 50,000 sawa na zaidi ya shilingi 115 za Kitanzania.

VIDEO: “ALISEMA KAMA SIO MIMI, WANANGU, HAWEZI KUENJOY” FAIZA ALLY, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA MWANZO MWISHO 

Soma na hizi

Tupia Comments