Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

Kauli iliyomkera Kanye West na kuamua kuwachana Jay Z na Beyonce Live Stejini

on

Licha ya kuwa washindani katika game ya mziki, Rapper Kanye West na familia ya Carter, Jay Z & Beyonce wamekuwa marafiki wakubwa tu kwa muda. Kanye West ameweka hilo pembeni na kufunguka kwamba hakupendezwa na kitendo cha Beyonce kusema hato perform kwenye tuzo za MTV Video Music Awards 2016 endapo video yake ya ‘Formation’ haitoshinda kama Video bora ya mwaka. Kanye aliyasema hayo alipokuwa kwenye show yake huko Sacramentino Carlifonia.

Beyonce alikuwa akishindanishwa na Kanye West pamoja na Drake kwenye kipengele hicho ambacho hata hivyo, alishinda. Kanye alisema alijisikia vibaya kusikia vile tena kama utakumbuka Kanye alishawahi kuingilia speech ya Tailor Swift mwaka 2009 alipopokea tuzo ambayo alisema alistahili  kuchukua Beyonce kitu ambacho kilimfanya asiwe na mahusiano mazuri na Taylor Swift.

Kanye aliendelea kwa kusema “sijaongea hivi ili muende kumdiss Beyonce, Beyonce ni mtu mahiri na hata Taylor Swift pia, mimi naongea tu mawazo yangu japokuwa wakati mwingine siasa zinatupelekea kujisahau”. Kanye alimalizia  kwa kumsihi Jay Z amcheki hewani waongee kama wanaume.

Baada ya kusema hayo Kanye alitupa Mic chini na kuondoka kwenye steji, kitu ambacho kililalamikiwa na mashabiki huku wakisema hawakwenda kutazama show ya nyimbo mbili tu.

 VIDEO: Alikiba na Ommy Dimpoz wakiimba ‘Kajiandae’ pamoja kwenye ON AIR na Millard Ayo>>>

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement