Top Stories

HEKAHEKA: Maamuzi ya familia baada ya kujua mtoto wao kauwawa na kuzikwa

on

Mtangazaji Geah Habibu kupitia kipindi cha Leo Tena ya Clouds FM leo Nov 27, 2017 ametuletea HekaHeka iliyotokea Moshi Kilimanjaro, inayohusu kifo cha mtoto wa kidato cha pili ambaye amekutwa na umauti wa kutatanisha akiwa shuleni ambapo awali ilisemekana ametoweka shule mara baadae akakutwa kashazikwa na manispaa.

Baba wa mtoto huyo ambaye alikuwa Dodoma amesema alipata taarifa ya kupotea kwa mtoto wake ndipo alipoenda kwenye shule hiyo lakini hakupewa taarifa zilikuwa za kuridhisha kutokana na maneno waliyokuwa wakisikia, badae wakasikia kuna mwili uliokotwa mtoni karibu na shule na kupelekwa hospitali kisha manispaa uliuzika mwili huo.

Baba wa mtoto alipofata taratibu waliufukua mwili huo uliokuwa umezikwa ambapo walikuta ni mtoto wake lakini mwanzoni kabla mwili haujazikwa inadaiwa kuwa aliitwa mwalimu kuukaguwa ambaye alisema hamjui mtoto huyo.

Bonyeza PLAY hapa chini kusikiliza Full Story..

HEKAHEKA: Geah Habib kamtafuta mjane aliyenyang’anywa mali na ndugu wa mume

Soma na hizi

Tupia Comments