Top Stories

“Sio vizuri kufunua makaburi, Bukoba tumewahi poteza bilioni 18” – Meya Bukoba

on

Leo December 31, 2017  ni Saa chache zimesalia kumaliza mwaka 2017 na kuingia 2018,  AyoTv na millardayo.com imempata Meya wa Manispaa ya Bukoba Chief Kalumuna ambapo ameeleza baadhi ya mambo waliyofanya kwa mwaka mmoja pamoja na vikwazo walivyokumbana navyo.

Kalumuna amesema kuwa kwa upande wao kama Madiwani wamefanya kazi bila kujali vyama vyao katika shughuli za kuleta maendeleo likiwemo swala la kujenga stend mpya na ya kisasa katika maeneo ya Kyakairabwa na wanatarajia kufikia February 2018 itakuwa imekamilika.

Aidha amesema kuwa kipindi cha nyuma waliwahi kupoteza fedha takribani Bilion 18 kutoka Benki ya Dunia  na hiyo ilitokana na kutoelewana kwa baadhi ya viongozi wa kisiasa ndani ya Manispaa.

BREAKING: TRA kuanza kumchunguza Askofu Kakobe “nina hela kuliko Serikali”

Soma na hizi

Tupia Comments