Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Top Stories

Shabiki amuachia Sanjay Dutt mali zake zote

on

Miongoni mwa stori iliyo-trend nchini India March 11, 2018 ni kumhusus Mwanamke mmoja kwa jina la Nishi Harishchandra Tripathi amefariki dunia na kumuachia mali zake zote nyota wa bollywood Sanjay Dutt.

Mwanamke huyo aliekuwa akiishi Mumbai alifariki January  15 baada ya kuugua. Gazeti la Mumbai Mirror limeandika kuwa mwanamke huyo siku chache kabla ya kufariki kwake aliamua kumuachia mali zake zote muigizaji aliekuwa akimpenda sana Sanja Dutt.

Sanjay Dutt alijawa na furaha baada ya kufahamishwa kuwa shabiki wake asiemfahamu amefariki na kumuachia urithi wake wote.

Hata hivyo Sanjay Dutt amesema kuwa hawezi kuzikubali fedha hizo na kuwa mwanasheria wake tayari ameanza taratibu za kuuhamisha urithi huo kwa familia ya marehemu.

Nishi Harishchandra Tripathi alifariki akiwa na umri wa miaka 62. Sanjay Dutt mwenye umri wa miaka 58 ni kati ya nyota maarufu sana wa filamu za kihindi na ameshaigiza katika filamu zaidi ya 100. 

SANJAY DUTT AITEMBELEA TANZANIA, AHOJIWA NA AYO TV

Soma na hizi

Tupia Comments