Tangaza Hapa Ad

Magazeti

Jamaa aliyemtahiri mwanawe kwa kisu kortini Bunda

on

Kila asubuhi Millard Ayo atazisogeza karibu yako habari zote kubwa kutoka kwenye Magazeti mbalimbali ya Tanzania ambapo huwa naziweka kwenye page ya Twitter ya @millardayo na kwenye Youtube ya millardayo bila kusahau millardayo.com.

Moja ya habari iliyoandikwa kwenye magazeti ya leo ni pamoja na hii ya kwenye gazeti la Habari leo yenye kichwa cha habari ‘Amjeruhi vibaya mwanawe kwa kumtahiri kwa kisu’

Gazeti hilo limeripoti kuwa mkazi wa kijiji cha Mihingo wilayani Bunda mkoani Mara, Marwa Elias amefikishwa mahakama ya wilaya ya Bunda kwa tuhuma ya kumtahiri vibaya kwa kutumia kisu, kukata kipande kikubwa cha uume wa mtoto na kumsababishia madhara makubwa mwilini mwake. 

Kwa sasa mtoto anajisaidia haja ndogo kwa shida kutokana na kukatwa sehemu hiyo ya siri vibaya. Inadaiwa baada ya tendo hilo mtuhumiwa huyo alitoweka na kwenda kwenye shughuli zake akimuacha mtoto huyo akiwa kwenye hali hiyo, baadaye hivi karibuni alikamatwa na kufikishwa polisi na kisha mahakamani.

Baada ya kusomewa shtaka lake mtuhumiwa alikana kutenda kosa hilo na kupelekwa mahabusu katika gereza la Nyasura nje kidogo ya mji wa Bunda, baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Unaweza kuzipitia hapa chini habari nyingine kubwa zilizoandikwa 

AyoTVMAGAZETI: IMF yaeleza hali ya uchumi waTZ, Manusura wasimulia ajali ya Jahazi Tanga 

Unazitaka Breaking NEWS na Stori zote? ungana na Millard Ayo kwenye Facebook Twitter Instagram na Youtube na atakuletea matukio yote ya picha, video na habari iwe usiku au mchana…. bonyeza hapa >>> FB Twitter Instagram YouTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement