Tangaza Hapa Ad

Mix

Majibu ya ACT Wazalendo kwa Ole Sendeka baada ya kutaka Zitto achunguzwe

on

Jana October 28 2016, msemaji wa chama cha mapinduzi ‘CCM’ Christopher Ole Sendeka alikutana na waandshi wa habari pamoja na mambo mengine Christopher Ole Sendeka alimshutumu Zitto Kabwe kwa kile alichosema amekuwa na chuki na serikali ya awamu ya tano, huku akidai alikuwa ni miongoni mwa viongozi waliokuwa wanasimamia shirika la NSSF wakati akiwa mwenyekiti wa PAC  ambalo hivi karibuni shirika la NSSF limekumbwa na kashfa ya ufisadi hivyo Ole Sendeka ametaka Zitto achunguzwe.

Baada ya tuhuma hizo chama cha ACT Wazalendo kimekutana na waandishi wa habari leo October 29 2016 kupitia kwa katibu wa bunge na Serikali za mitaa wa ACT Wazalendo, Habibu Mchange ambapo amesema wameshtushwa  na tuhuma hizo zilizotolewa na  msemaji wa chama cha Mapinduzi ‘CCM’, Christopher Ole Sendeka dhidi ya Kiongozi wa chama chao,  Zitto Kabwe,  hivyo kutokana na hayo chama cha chao kinakaribisha uchunguzi juu ya mali za Zitto.

>>>’Chama chetu kinakaribisha uchunguzi juu ya mali na madeni ya Kiongozi wetu, ndugu Zitto. Tutafurahi uchunguzi huo ukihusisha akaunti zake za benki pamoja na mfumo wa maisha yake binafsi’:-Habibu Mchange

>>>’Tunavitaka vyombo vya uchunguzi vianze kazi hiyo mara moja kwani tunaamini kuwa  Kama kuna Kiongozi ambaye Mali, Madeni, Maslahi na akaunti zake viko wazi basi ni ndugu Zitto. Ikumbukwe kuwa Katiba na Kanuni za chama chetu huwataka Viongozi wote wa chama kuweka hadharani tamko la mali zao na madeni, ndugu Zitto alitekeleza matakwa hayo ya kisheria, na mali pamoja na madeni yake yako hadharani na mtandaoni’-Habibu Mchange

 

ULIKOSA CCM KUTAKA ZITTO ACHUNGUZWE? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement