Michezo

UEFA imeiadhibu Man United kwa uzembe wa dakika 5

on

Shirikisho la soka Ulaya UEFA leo Ijumaa ya October 19 2018 imefikia maamuzi ya kuiadhibu club ya Man United ya England kutokana na kuzembea kidogo katika suala la muda wakati wa game za UEFA Champions League msimu wa 2018/2019.

UEFA wamefikia maamuzi ya kuiadhibu Man United kwa kuipiga faini ya Tsh Milioni 39 kutokana na timu ya Man United kuchelewa kufika uwanjani kwa dakika tano wakati wa mchezo wa hatua ya makundi wa UEFA Champions League dhidi ya Valencia.

Kuchelewa kwa wachezaji wa Man United kufika uwanjani, kulipelekea mchezo dhidi ya Valencia kuchelewa kuanza kwa dakika tano hivyo kwa mujibu wa kanuni za UEFA wanastahili adhabu kama waliyopewa.

Samatta alivyofutwa miguu baada ya game

Soma na hizi

Tupia Comments