PremierBet Ad
Asas Dairies Ad
NBC Ad

Michezo

Wengine waliotangaza ofa ya nusu bei baada ya Paul Makonda, inaanzia saa 2 asubuhi – 8 mchana

on

Kila Mtanzania ana furaha na ushindi wa Taifa Stars kuwafunga Uganda 3-0 ambapo ofa zilianza za nusu bei zilianza kutolewa hata kabla ya mechi ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda aliahidi vinywaji kuuzwa nusu bei kwenye Baa zote iwapo Stars itashinda, sasa baada ya ushindi wengine waliotangaza nusu bei wamejitokeza….. ni Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili DSM.

Taasisi hiyo imetangaza nusu bei yao ya matibabu kwa Wagonjwa wa moyo ambapo taarifa yao imesema Tunaipongeza timu ya Taifa Stars kwa ushindi mlioupata. Kutokana na ushindi huo kesho trh 25/3/2019 kuanzia saa 2asb hadi saa 8 mchana wagonjwa wa kulipia watakaotibiwa JKCI watalipa gharama ya chini ya 25,000/= badala ya 120,000/= kwa vipimo vya ECHO, ECG na kumuona Daktari

“Tunaipongeza timu ya Taifa Stars kwa ushindi mlioupata, kutokana na ushindi huo kesho tarehe 25/3/2019 kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa 8 mchana Wagonjwa wa kulipia watakaotibiwa JKCI watalipa gharama ya chini ya 25,000/= badala ya 120,000/= kwa vipimo vya ECHO, ECG na kumuona Daktari”

TAIFA STARS WALIVYOISUBIRIA FILIMBI YA MWISHO 3-0

VIDEO: RAIS MAGUFULI ASEMA “LEO NIMEFURAHI SANA, LEO NDIO NIMEONA MPIRA SIO ULE WA SIKU ILE” BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUMTAZAMA JPM

Soma na hizi

Tupia Comments