PremierBet Ad
Asas Dairies Ad
NBC Ad

Michezo

Shaban Iddi wa Azam FC anaungana na Farid soka la kulipwa Hispania

on

Good news inazidi kutawala katika soka la bongo kufuatia taarifa njema kuwa soka la Tanzania linazidi kutoa wachezaji wake nje ya mipaka ya Afrika na kwenda kucheza soka la kulipwa Ulaya.

Taarifa zilizotolewa leo kuhusiana na mshambuliaji wa Azam FC Shaban Iddi Chilunda ni kuwa amefanikiwa kusaini mkataba wa miaka miwili wa kuichezea club ya CD Tenerife ya Hispania inayocheza Ligi daraja la kwanza nchini humo (Segunda Division).

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Chilunda sasa anaungana na mtanzania mwenzake Farid Musa ambaye alijiunga na club ya CD Tenerife miaka kadhaa iliyopita na amedumu nayo hadi leo hii.

Haji Manara kapenda usiku wa VPL ila kafunguka wasiwasi wake

Soma na hizi

Tupia Comments