Biko Ad
MPTV Ad
TIC Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

David Beckham kuhusu Sterling “Hii sikuiona haikuwa sahihi”

on

Imekuwa kawaida kwa baadhi ya watu au wachambuzi wa soka duniani au wachezaji wa zamani kupenda kuchambua soka na hata uwezo wa wachezaji wa kisasa, staa wa zamani wa Man United Garry Neville ni moja kati ya wachambuzi wa soka kwa sasa na amekosoa wanaomsema Raheem Sterling.

Baada ya staa wa zamani wa timu ya taifa ya England na club ya Man United David Beckham kuiona taarifa ya Neville akimtetea Raheem Sterling, ameandika kutumia ukurasa wake wa instagram akiambatanisha na habari ya Neville.

“Sikuwa nimeiona hii lakini kwa vyovyote vile hii sio sahihi tupo katika nusu fainali ya Kombe la Dunia sasa, kila mchezaji anastahili pongezi na kujivunia uwepo wake, kama nchi tumeungana kuisapoti timu”>>> Beckham

Sterling alikosolewa na baadhi ya watu kutokana na kiwango chake alichokionesha katika mchezo wa robo fainali wa England dhidi ya Sweden uliyomalizika kwa England kupata ushindi wa 2-0, July 11 2018 timu ya taifa ya England itacheza mchezo wake wa nusu fainali ya World Cup 2018 dhidi ya timu ya taifa ya Ubelgiji.

Haji Manara kapenda usiku wa VPL ila kafunguka wasiwasi wake

Soma na hizi

Tupia Comments