Michezo

Thomas Ulimwengu amevunja mkataba na Al Hilal

on

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania alieyekuwa anacheza soka katika club ya Al Hilal ya Sudan Thomas Ulimwengu, leo Jumatatu ya November 5 2018 zimeripotiwa taarifa za yeye kuvunja mkataba na club hiyo.

Taarifa hizo zilizoripotiwa na Azam TV kupitia kipindi cha Alasiri, Ulimwengu imeripotiwa kuwa amefikia maamuzi ya kuvunja mkataba na Al Hilal kutokana na kushindwa kutimiziwa makubaliano yao kama walivyokubaliana.

Mkataba wa Thomas Ulimwengu na Al Hilal unavunjika ikiwa imepita miezi mitano, tokea staa huyo ajiunge na Al Hilal kama mchezaji huru baada ya kukosa kibali cha kucheza Bosnia.

Hakuna anayemkuta Samatta kwa sasa Jupiter Pro League 2018/19

Soma na hizi

Tupia Comments