Biko Ad 2
MPTV Ad
TIC Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

DoneDEAL: Arsenal imemtangaza nyota wao mpya

on

Bado dirisha la usajili kwa vilabu mbalimbali duniani kote linaendelea na tumeona nyota kadhaa wametangazwa kujiunga na club mpya na wengine kuongeza mkataba katika vilabu vyao vya zamani.

Club ya Arsenal ambayo ipo na kocha mpya kwa sasa Unai Emery baada ya utawala wa miaka 22 ya kufundishwa na kocha Arsene Wenger, leo imeendeleza kuboresha kikosi chake kwa kutangaza usajili mpya chini ya kocha wao mpya Unai Emery.

Arsenal leo imetangaza kumsajili Lucas Terreira kutokea club ya Sampdoria ya Italia na tayari wamemtambulisha rasmi mbele ya waandishi wa habari na kumkabidhi jezi namba 11, Lucas amesajiliwa kwa dau linalotajwa kufikia pound milioni 26.

Haji Manara kaeleza sababu za kuwasajili Wawa, Dida na Kagere

Soma na hizi

Tupia Comments