Top Stories

Alichozungumza Rais Magufuli leo akiwa kwenye Ibada Dodoma

on

President John Pombe Magufuli leo December 17, 2017  ameungana na waumini wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo wa Msalaba Jimbo Kuu Katoliki mkoani Dodoma  katika ibada ya Jumapili.

President Magufuli amezungumza na waumini wa kanisa hilo baada ya Ibada na kuwashukuru viongozi wote wa dini na waumini wa madhehebu mengine kwa kuendelea kuliombea Taifa amani, JPM ameeongozana na mkewe Janeth Magufuli katika ibada hiyo.

JPM amesema Serikali anayoiongoza inatambua juhudi zinazofanywa na viongozi wa Dini katika kudumisha amani na upendo amehaidi serikali yake kuendelea kushirikiana nao katika kujenga Tanznia bora.

“Nawaomba viongozi wa madhehebu yote ya dini tuendelee kuliombea Taifa letu liwe na amani na upendo, serikali itashirikiana nanyi muda wote,” – Rais JPM

Katika ibada hiyo Rais JPM amechangia ujenzi Kigango cha Michese na kwaya ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo wa Msalaba kiasi cha shilingi milioni 3.

Baada ya maneno hayo ya Rais JPM, Padre wa Kanisa hilo  Sergio Madinda amemshukuru Rais Magufuli kwa ushirikiano wake na kanisa hilo na pia amemshukuru kwa kuhamishia Serikali mkoani Dodoma

BREAKING: RAIS MAGUFULI APITISHWA KUGOMBEA TENA CCM BAADA YA TAFAKURI YA KINA, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA

 

 

Soma na hizi

Tupia Comments