Habari za Mastaa

Hatimaye Lil Wayne kupewa tuzo ya heshima ‘I am Hip Hop’

on

Kwa mujibu wa mtandao wa Hip Hop Dx umeripoti kuwa Rapper Lil Wayne atapokea tuzo ya heshima ya ‘I am Hip Hop’ atakayopewa kwenye tuzo za BET Hip Hop zitakazofanyika October 6,2018 Marekani.

Lil Wayne atapokea tuzo hiyo ya heshima kutokana na kuwahi kuuza zaidi ya nyimbo 100 ikiwa pia amewahi kuwa msanii wa kiume wa kwanza kuzipita rekodi za Elvis Presley katika chart ya Billboard Hot 100 na jina lake kutokea mara 138 katika chart hizo.

Mashabiki wanasubiri kwa hamu ujio wa Album mpya ya Lil Wayne “Tha Carter V “ ambayo inatajwa kuwa sokoni September 21,2018, Album hiyo imekuwa ikishikiliwa kwa miaka mingi kutokana na mivutano ya kisheria iliyokuwepo kati yake na kundi la Cash Money.

SAKATA la Maua Sama lilivyowagusa Mastaa wa Bongo

Soma na hizi

Tupia Comments