Habari za Mastaa

PICHA 4: Kanye West & Kim Kardashian ndani ya Ikulu ya Uganda

on

Rapper Kanye West pamoja na mke wake Kim Kardashian wamepata nafasi ya kukutana na Rais wa Uganda Yoweri Museven leo October 15,2018 wakiwa ndani ya Ikulu ya nchi hiyo, rappa huyo pia kampatia Rais Museven zawadi ya viatu vya Yeezy.

Kanye West pamoja na familia yake waliwasili Uganda Jumamosi ya October 13,2018 na kufikia hoteli ya kifahari yenye hadhi ya nyota tano Chobe Safari Lodge na inaelezwa kuwa tayari Kanye West kashaanza kufanya kazi na record label ya Swangaz Avenue kwaajili ya kukamilisha Album yake ya ‘Yandhi’.

Inadaiwa kuwa ni wiki moja imepita tokea Kanye West abadilishe jina lake na kujiita ‘Ye’ na kujitoa katika mtandao wa Instagram pamoja na Twitter bila kutaja sababu ya kufanya hivyo.

“Wema Sepetu niliweka Dola mezani akaila”-Idris Sultan

Soma na hizi

Tupia Comments