Habari za Mastaa

VIDEO: Mke wa Ludacris aikubali ngoma ya Rich Mavoko ‘Rudi’

on

Mke wa msanii na muigizaji wa Marekani Ludacris ameonekana kukumbuka Afrika ambapo ndio asili yake maana ana uraia wa Gabon na kuonekana akiburudika na wimbo wa ‘Rudi’ wa Rich Mavoko pamoja na ngoma ya ‘Sitya Loss’ ya Eddy Kenzo kutokea Uganda.

Mke wa Ludacris ambaye jina lake ni Eudoxie Mbouguiengue amepost videos zikimuonyesha aki-enjoy ngoma hizo kupitia insta story yake kwa upande wa wimbo wa Rich Mavoko, Eudoxie ameonekana kukariri baadhi ya maneno ya Kiswahili kutoka kwenye ngoma hiyo ambayo iliachiwa rasmi November 1, 2017 kupitia mtandao wa You Tube.

Eudoxie Mbouguiengue alifunga ndoa na Ludacris mwaka 2014, na wamebahatika kupata mtoto mmoja wa kike aitwae Cadence na wanaishi pamoja nchini Marekani.

EXCLUSIVE: MUME WA LINNAH KAFUNGUKA “TUMESHINDWANA MIMI NAE, USALITI”

Soma na hizi

Tupia Comments