Biko


Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

Maagizo ya simu aliyopiga Rais Magufuli kwenye FIESTA leo Alfajiri

on

Habari kubwa ya November 25 2017 Tanzania ilikua ni Tamasha kubwa la Muziki wa Bongofleva (FIESTA 2017) lililofanyika viwanja vya Leaders Club Dar es salaam ikiwa ni Fainali ya tamasha hilo kwa mwaka 2017.

Ni Tamasha ambalo mwanzoni ilitangazwa lingemelizika saa saba kamili usiku ambapo baadae ikatangazwa kibali kimetolewa mpaka saa kumi na moja Alfajiri.

Ilipofika saa kumi na moja Alfajiri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli alipiga simu na kusema tamasha hilo lifanyike mpaka saa kumi na mbili kamili asubuhi ambapo hapa chini nanukuu kilichoandikwa kwenye page ya CloudsFM.

“Tumepokea simu kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli amesema #TigoFiestaKubwaLao iende hadi saa 12 asubuhi. Yani akienda Kanisani anapishana na watu wanatoka Fiesta”

“Sisi tunashukuru sana, Asante sana Rais wetu kwa kuonyesha upendo kwa kiwanda cha burudani, tutaendelea kusimamia tasnia hii kwa maslahi ya Taifa letu #BabaKasema #JPMnaMuziki “

VIDEO: WASANII WALIVYOINGIA KWA MKWARA KWENYE FIESTA 2017 LEADERS CLUB DSM, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA

WAMERUDIANA !! MAHABA YA JUX….. VANESSA KAKUBALI MSAMAHA MWENYEEEEEWE, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUMTAZAMA

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement