Michezo

Tottenham na Real Madrid wameianza vizuri 16 bora ya Champions League

on

Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora imeendelea usiku wa February 13 2019 kwa michezo miwili kucheza, Tottenham Hotsputs walikuwa Borussia Dortmund wakati Ajax walikuwa wenyeji wa Real Madrid.

Game ya Tottenham akiwa nyumbani wamefanikiwa kuifunga Borussia Dortmund kwa magoli 3-0, magoli ya Tottenham yakifungwa na Son Heung-Min dakika ya 47, Vertoghen dakika ya 83 na Llorente dakika ya 86, wakati game ya Real Madrid ilimalizika kwa wao kupata ushindi wa magoli 2-1, yaliofungwa na Karim Benzema dakika ya 60 na Marco Asensio dakika ya 87 huku Ajax wakifuta machozi kwa goli la Ziyech dakika ya 75.

Game za marudiano ili kuingia robo fainali kwa Tottenham watahitaji sare ya aina yoyote au kupoteza mchezo kwa chini ya magoli matatu wakati Real Madrid wao wakihitaji sare nyumbani ili wasonge mbele, Ajax na Dortmund watakuwa na mtihani mzito wa kupindua matokeo mechi za marudiano.

Imeshinda Simba SC tabu kaipata JB wakati wa kutoka

Soma na hizi

Tupia Comments