Tangaza Hapa Ad

AyoTV

AUDIO: Ni kweli kuna uhusiano wa kupatwa kwa jua na tetemeko la ardhi?

on

Baada ya kuwepo kwa taarifa mbalimbali zilizoripotiwa na vyombo vya habari zikidai kuwa Tukio lililotokea September mosi mwaka huu la kupatwa kwa jua Mbarali lina uhusiano na tetemeko la ardhi lililotokea mikoa ya kanda ya ziwa na kuleta madhara makubwa kwa wakazi wa Kagera ambapo mpaka sasa vimeripotiwa vifo 17.

millardayo.com na Ayo TV imempata mjiolojia mwandamizi wa wakala wa jiolijia Tanzania, Gabriel Gomboni kwa majibu kama ni kweli kuna uhusiano wowote wa tukio la kupatwa kwa jua na tetemeko la ardhi …….

‘Kwa kweli hakuna uhusiano wowote wa kupatwa kwa jua na tetemeko la ardhi, tetemeko la ardhi linasababishwa na process ambazo zinatokea katika kina kirefu cha ardhi ambapo huo ni mgandamizo unaotokana na nguvu za asili kwenye miamba, huo mgandamizo unafikia pointi ile miamba inashindwa kuhimili ule mgandamizo na kupelekea kukatika kwa miamba inayosababisha ardhi kutikisika’

ULIKOSA UFAFANUZI KUHUSU VIPIMO VYA MATETEMEKO YA ARDHI VILIVYOIBIWA? BONYEZA PLAY HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement