Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Pep Guardiola ametangaza hatma ya Yaya Toure Man City

on

Kiungo wa kimataifa wa Ivory Coast Yaya Toure alijiunga na Man City mwaka 2010 akitokea FC Barcelona ya Hispania aliyodumu nayo kwa miaka mitatu, Toure mwenye umri wa miaka 34 kwa sasa hatma yake ndani ya club ya Man City inakaribia mwisho baada ya kocha wake Pep Guardiola kutoa taarifa hizo kwenye vyombo vya habari.

Baada ya Yaya Toure kujiunga na Man City alikuwa moja kati ya wachezaji muhimu katika kikosi cha Man City lakini msimu huu akiwa na umri wa miaka 34 amekuwa na wakati mgumu kupata nafasi kikosi cha kwanza na kocha wake Pep Guardiola amethibitisha kuwa Toure ataondoka Man City mwishoni mwa msimu huu.

“Yaya Toure hatosalia Man City msimu ujao, game dhidi ya Brighton tunapambana kushinda kwa ajili ya  Yaya, Toure alikuja hapa kuanzisha safari pamoja na hata hapa tulipo kwa sasa ni kwa sababu ya kazi yake aliyoifanya alikuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Man City”>>>Pep Guardiola

Bado haijajulikana Yaya Toure atakwenda timu gani baada ya kuondoka Man City atastaafu au ataendelea na soka lakini kama ufahamu Yaya Toure alianza kucheza soka mwaka 1996-2001 kuanzia akiwa na umri wa miaka 13 hadi 18 katika club ya ASEC Mimosas ya kwao Ivory Coast na baadae alienda Ubelgiji kucheza BeverenFC Metalurh Donetsk ya Ukraine, Olympiacos ya Ugiriki na AS Monaco ya Ufaransa.

VIDEO: Mbwembwe za Haji Manara uwanjani baada ya ushindi wa Simba vs Yanga

Soma na hizi

Tupia Comments