Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Masoud Djuma kafunguka, kajiuzulu Simba SC?

on

Baada ya kusambaa kwa taarifa katika mitandao ya kijamii zikidai kuwa kocha msaidizi wa Simba SC raia wa Burundi Masoud Djuma amejiuzulu nafasi yake hiyo, mwenyewe amefunguka.

Kupitia ukurasa wa instagram wa msemaji wa Simba SC Haji Manara, Masoud Djuma amekanusha taarifa hizo na kusema yeye Simba haondoki leo wala kesho labda afukuzwe kwani bado ana mkataba na Simba SC.

“Kwanza naomba nikanushe taarifa hizo wala sijui zinatoka wapi mimi Masoud Djuma ni kocha msaidizi wa Simba SC, nina mkataba Simba sina mawazo ya kusema leo kesho nitaondoka labda wanifukuze”-Masoud Djuma

Soma na hizi

Tupia Comments