Michezo

Simba imewadhihirishia Azam FC kuwa imeamua kutetea Ubingwa wa TPL

on

Simba SC inaendelea kucheza michezo yake ya viporo vya Ligi Kuu soka Tanzania bara msimu  wa 2018/2019, hiyo baada ya kubanwa na michezo ya kimataifa ya CAF Champions League, Simba leo walikuwa wageni wa Azam FC uwanja wa Taifa Dar es Salaam, Simba wakitafuta point kutetea taji hilo na Azam FC wantaka ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kulitwaa taji hilo.

Leo Azam FC wakiwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam wamejikuta wakikubali kipigo cha magoli 3-1 kutoka Simba huku wao wakiishia goli moja la kufutia machozi lililofungwa na Frank Domayo dakika ya 81, Simba SC walipata magoli yao na kuchukua point tatu kupitia kwa Meddie Kagere aliyefunga magoli mawili dakika ya 4 na 77 na baadae John Bocco ambaye ni nahodha nae alifunga goli la pili dakika ya 38.

Simba ambao bado wana viporo vya kutosha walicheza mchezo huo wakifanikiwa kuutawala kwa asilimai 59 kwa 42 dhidi ya Azam FC, huku Azam FC wakiishia kupiga mashuti mengi kwa Simba (12) yasioweza kulenga lango wala kuwapa matokeo, Azam FC anaedelea kuwa nafasi ya pili nyuma ya Yanga kwa kuwa na point 50 akicheza michezo 24 wakati Simba akiwa nafasi ya tatu kwa kuwa na point 45 wakicheza michezo 18 wakiwa na viporo michezo 7.

Mwinyi Zahera alisababisha shabiki wa Yanga abet mke wake

Soma na hizi

Tupia Comments