Tangaza Hapa Ad

Mix

VIDEO: Yanayojiri nyumbani kwa Mzee Sitta na ratiba ya mazishi

on

Viongozi mbalimbali wa serikali na wakazi wa Dar es salaam wameuaga mwili wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samuel John Sitta aliyefariki dunia tarehe November 07  2016 katika hospitali ya Technical University of Munich nchini Ujerumani.

Baada ya kuagwa katika viwanja vya Karimjee, mwili wa Marehemu Samuel John Sitta umesafirishwa kwenda Dodoma ambako Wabunge, Viongozi wa Mkoa na wananchi watapata fursa ya kuuaga katika Viwanja vya Bunge na baadaye jioni utasafirishwa kwenda Tabora ambako maziko yatafanyika kesho Jumamosi huko Urambo.

Ripota wa AyoTV na millardayo.com yupo Urambo Tabora kuhakikisha anakuletea kila kinachojiri nyumbani kwa marehemu mzee Sitta na maandalizi ya kuupokea mwili huo wa mbunge mstaafu wa Urambo.

Nimekuwekea video ya maandalizi ya msiba ambapo mwili wa marehemu unatarajiwa kuwawasili uwanja wa ndege Tabora kuanzia saa kumi na moja jioni na kupelekwa Urambo nyumbani kwake na baadaye wananchi wa Urambo watapata fursa ya kuagana na mpendwa wao Mzee Sitta na atazikwa katika makaburi ya watu wengi ambapo kuna eneo la kuzikwa familia ya Sitta ambayo ipo umbali wa km 2 kutoka nyumbani kwake.

VIDEO: Mwili wa Samuel Sitta ulivyoagwa Karimjee DSM. VIDEO HII HAPA CHINI

Tupia Comments

Advertisement