Tangaza Hapa Ad

AyoTV

VIDEO: ‘Tuifumue tuweke watu wazuri zaidi tena sitaki wazee’;- Waziri Mbarawa

on

Leo November 16 2016 Waziri wa mawasiliano, uchukuzi na ujenzi, Prof. Makame Mbarawa kwa mara ya kwanza ametembelea kampuni ya reli Tanzania ‘TRL’ kwa ajili ya kuzindua bodi mpya ya TRL pia aliongea na wafanyakazi wa kampuni hiyo.

Wakati akizungumza na wafanyakazi Waziri Mbarawa amelitaja suala la masoko kuwa changamoto kubwa TRL ambapo ameagiza Idara ya masoko kufumuliwa.

>>>’Utafutaji wa masoko bado hauko vizuri nataka idara ya masoko tuifumue tuweke watu wazuri zaidi tena sitaki wazee, wadogo tunawasukuma wafanye kazi sisi wazee tutakaa nyuma tunawaangalia vijana wanafanyaje  lakini idara ya masoko lazima tuifumue vijana waende wakatafute masoko’

>>>’Idara ya masoko nataka upange vijana wazuri ambao wataipeleka TRL, TRL ni masoko tu ukipata masoko vizuri umemaliza, biashara yoyote siku hizi ni masoko ukipata masoko vizuri, ukiwahudumia wateja vizuri umemaliza kazi, nataka tupate watu wazuri kwenye masoko watu watakaokuletea shida waleta tutawafukuza ‘

VIDEO: ‘Maamuzi niliyoyatoa bungeni mengine yalikuwa hayanipendezi hata mimi’- Dk Tulia Ackson 

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement