Top Stories

Kauli ya Chadema juu ya kesi yao na Zitto Kabwe leo.

on

DSC_0168

Bado kesi ya Chadema na mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe inaendelea baada ya Jaji kuahirisha kesi hii ambayo imeonekana kuwa na msuguano wa kisheria pande zote mbili, upande wa Chadema waliweka mawakili watatu Peter Kibatala, John Marya wakiongozwa na wakili wa Chadema Tundu Lissu.

lissu2

Upande wa Zitto Kabwe ni mwanasheria wake wa siku zote Albert Gasper Msando ambaye pia ni diwani wa kata ya Mabogini kupitia Chadema huko 87.9 Moshi ambapo baada ya leo kuahirishwa kesi yao mpaka Jan 6 2013, millardayo.com imeongea na Tundu Lissu ambae ni Mwanasheria wa Chadema.

‘Nafikiri tumeenda vizuri pande zote mbili zimepigana kwa ufundi mkubwa sana nafikiri Jaji ana kazi kubwa sana kesi imehairishwa mpaka Jumatatu kwa sababu masuala yaliyojadiliwa ni masuala mazito sana kisheria yanahitaji muda wa Jaji kufanya utafiti na kuyatafakari, nawaambia Wanachadema chama chetu kipo imara hili wingu litapita lakini ni muhimu wafahamu mahali ambapo tumefika leo, chama lazima kisafishe uchafu wote ndani ya chama utovu wote wa nidhamu uondolewe chama lazima kijisafishe vinginevyo hatutoweza kama tutaendekeza usaliti na kelele za aina hii, ujinga wa aina hii chama kitasambaratika’

‘Mimi sidhani kama kuna makundi mawili, kwenye kamati kuu nzima wajumbe zaidi ya 30 wote wameungana na hicho ndio chombo cha juu kabisa cha kufanya maamuzi ya chama, kuhusu baraza kuu kikao cha mwisho kabisa cha mwaka jana January, Mwenyekiti wa chama ilibidi azime mjadala uliokua kwenye baraza kuu kumhusu mheshimiwa Zitto Kabwe, wajumbe wa baraza kuu walikua wanasema huyu mtu aondoke toka mwaka jana kwa hiyo haya maneno kuwa baraza kuu tunaenda kushinda ni maneno yaleyale kwamba kwenye kamati kuu tupo wengi tuna akili nyingi hawatotugundua tumesoma hawa wengine hawajasoma akili ndogo’

Tupia Comments