Tangaza Hapa Ad

AyoTV

VIDEO: Kuhusu taharuki ya Moto uliolipuka kwenye bandari ya DSM

on

Leo Nov 1 2016 katika Bandari ya Dar es salaam kumetokea moto ambao umezua taharuki kwa baadhi ya wafanyakazi na watu wengine waliokuwa eneo hilo la bandari. Moto huo uliolipuka kwenye makontena na kuteketeza kontena tatu zilizokuwa na matairi ya magari na kudumu kwa muda wa dakika 30.

Mkuu wa mawasiliano wa mamlaka ya Bandari, Peter Mlanzi ametoa ufafanuzi kuhusu moto huo kwamba umeandaliwa makusudi kwa ajili ya kukipima kikosi cha zima moto…….>>>’tukio hili tumelitengeza kwa makusudi ili tuone namna ambavyo  kikosi kazi cha zimamoto na uokoaji kinavyoweza kukabilana na majanga mbalimbali’

Aidha kwa upande wake mkuu wa kikosi cha zimamoto bandari ya Dar es salaam, Mussa Biboze, amesema…..>>>’kwa zimamoto moto uko kwenye madaraja, huu moto wa matairi ni moto wa daraja A ambao unazimwa tu na maji ya kawaida

ULIKOSA HII AJALI YA MOTO ILIYOTOKEA USIKU WA MANANE DAR ES SALAAM?  ITAZAME HII VIDEO HAPA CHINI..

 

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement