Tangaza Hapa Ad

Michezo

Kiungo wa Tottenham ya England kaguswa na tetemeko la Bukoba

on

Taifa la Tanzania bado lipo katika majonzi na masikitiko makubwa, kufuatia maafa ya tetemeko la ardhi yaliotokea Bukoba mkoani Kagera, baadhi ya wafanyabiashara makampuni na taasisi tofauti tofauti zimeoneshwa kuguswa kwao kutokana na tetemeko hilo lililogharimu uhai wa baadhi ya watanzania.

victor-wanyama-spurs_3489343

Tanzania imekuwa ikipokea pole nyingi kutoka sehemu mbalimbali duniani, moja kati ya watu maarufu walioguswa na tukio hilo ni kiungo wa kimataifa wa Kenya anayecheza klabu ya Tottenham Hotspurs Victor Wanyama ametumia ukurasa wake wa twitter kuungana na watu wa Bukoba na Tanzania.

victor-wanyama

Wanyama ambaye kwa sasa yuko London Egland kwa ajili ya kuitumikia Tottenham Hotspurs katika michezo ya Ligi Kuu na leo Septemba 14 katika mchezo wao wa kwanza wa Kundi E wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Monaco katika uwanja wao wa White Hatlane ameandika ujumbe ufuatao katika ukurasa wake rasmi wa twitter.

“Fikra zangu na maombi yangu kwa watu wa Tanzania na Bukoba kufuatia majanga ya tetemeko la ardhi lilitokea #TukoPamoja”

ALL GOALS: Simba vs AFC Leopard August 8 2016, Full Time 4-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement