Habari za Mastaa

Gigy Money aweka wazi magumu aliyopitia akiwa mapenzini na Mo J

on

Mwimbaji Gigy Money amefunguka kuhusiana na aliyekuwa mpenzi wake Mtangazaji wa Clouds Radio Mo J na kusema kuwa kipindi yupo mapenzini alikuwa akivumilia vitu vingi kutoka kwa Mwanaume huyo ikiwa pamoja na kupigwa ila alihisi ipo siku atabadilika.

Gigy Money amegusia pia ishu ya kujihusisha na wanaume mbalimbali ili kumsahau Mo J lakini haikumsaidia na kusema kuwa alifanya hivyo ili kuhahakisha Mwanae Myra anapata baba bora na hakutaka mwanae apitie yote aliyokuwa akipitia kwa wakati huo.

Gigy Money ameyaandika hayo kupitia ukurasa wake wa instagram huku akitaka watu wanaomuita malaya waelewe alichopitia wakati yupo na Mo J .

MZEE WA ‘KONKI LIQUID, KONKI FIRE’ ‘AFIKA’ NIGERIA

Soma na hizi

Tupia Comments