Michezo

“Sio sisi tuliomkataa tumepokea barua kutoka Yanga”-Rais wa TFF

on

Rais wa shirikisho la soka Tanzania TFF Wallace Karia amefunguka na kueleza kuhusiana na maamuzi ya kamati ya utendaji wa TFF kumuondoa Frank Sanga wa Yanga katika nafasi ya uenyekiti wa bodi ya Ligi.

Wallace Karia ameeleza kuwa sio wao TFF ndio wameamua kumuondoa katika nafasi hiyo ila kanuni na sheria ndio zinamn’goa Sanga katika nafasi hiyo, kwani wamepokea barua kutoka Yanga ikithibitisha kuwa Yussuf Manji ndio mwenyekiti wa Yanga na Sanga ni makamu mwenyekiti.

Frank Sanga

Hivyo sheria inaeleza kuwa ili uwe mwenyekiti wa bodi ya Ligi au mjumbe ni lazima uwe mwenyekiti wa club yako, hivyo Sanga ambaye alikuwa kaimu mwenyekiti wa Yanga baada ya kurudi katika nafasi yake ya makamu mwenyekiti, basi anapoteza sifa za kuendelea kuwa mwenyekiti wa bodi ya Ligi.

Haji Manara kaeleza sababu za kuwasajili Wawa, Dida na Kagere

Soma na hizi

Tupia Comments