Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Wachezaji wa Real Madrid wamepiga picha za jezi mpya, Ronaldo vipi?

on

Siku chache baada ya club ya Real Madrid kutwaa taji lao la 13 la Ligi ya Mabingwa Ulaya maarufu kama UEFA Champions League, wachezaji wa Real Madrid wamepiga picha wakiwa katika muonekano wa jezi zao mpya zilizotengenezwa na kampuni ya Adidas na Real Madrid wataanza kuzitumia jezi hizo katika msimu wa 2018/2019.

Moja kati ya stori zilizochukua headlines baada ya kupigwa kwa picha hizo ni kutokana na kukosekana kwa staa wa timu hiyo Cristiano Ronaldo, wachezaji wengi wa Real Madrid wameonekana katika picha hizo kasoro Ronaldo ambapo amezua maswali kuwa kuna uwezekano asiwe na Real Madrid msimu ujao.

Imekuwa kawaida au utamaduni wa kawaida kwa wachezaji wenye majina makubwa ndani ya club kutumika katika kutambulisha jezi mpya za club lakini kama anakosekana huwa ni dalili kuwa msimu ujao kuna uwezekano asiwepo katika club hiyo, Ronaldo baada ya kutwaa Champions League alinukuliwa akisema siku zijazo atatangaza hatma yake.

Yametimia maneno ya mchambuzi mkongwe Dr Leaky kuhusu Champions League

Soma na hizi

Tupia Comments