AyoTV

Kocha wa Simba katangaza muda atakaokuwa nje ya uwanja Erasto Nyoni

on

Kocha Mkuu wa Simba SC Patrick Aussems leo ameongea na waandishi wa habari kuelekea mchezo wake wa mwisho wa hatua ya Makundi Mapinduzi Cup 2019 dhidi ya Mlandege utakaochezwa saa 20:00 lakini pia na game yao ya CAF Champions League dhidi ya JS Saouro ya Algeria.

Patrick Aussems amesema hajapata nafasi ya kuwaona wapinzani wake JS Saouro lakini alituma marafiki zake akawaangalia na kujua walivyo, hivyo anajua namna ya kuingia katika mechi hiyo ya nyumbani ila kuhusu Erasto Nyoni kocha ameeleza kuwa amefanyiwa vipimo na atakuwa nje ya uwanja kwa wiki tano.

Mpenja katangaza goli kabla ya kona kupigwa, ataomba kutotangaza game za timu yake

Soma na hizi

Tupia Comments