PremierBet Ad
Asas Dairies Ad
NBC Ad

Habari za Mastaa

R. Kelly aiomba Mahakama imruhusu kwenda Dubai

on

Inaripotiwa kuwa mwimbaji wa RnB R. Kelly yupo nje kwa dhamana huku akisubiri kusikilizwa mashtaka yake 10 ya ishu inayomuandama juu unyanyasaji wa kingono kwa wasichana wadogo inayomkabili.

Kwa mujibu wa mtandao wa The Blast umeripoti kuwa R. Kelly ameiomba Mahakama kumpatia ruhusa ya kusafiri kwenda nchini Dubai kwaajili ya kutumbuiza kwenye maonesho yake kadhaa yaliyopangwa kufanyika mwezi April 17 hadi 19 mwaka huu 2019 pamoja na kukutana na familia ya kifalme.

Inaelezwa pia R Kelly ana mpango wa kufanya matamasha  3 mpaka 5 nchini Dubai, huku Uongozi wake umeweka wazi kuwa mwimbaji huyo alikubali kufanya show hizo kabla hata ya kukamatwa

VIDEO: MC PILIPILI “SIKUWAI KUPATA MZURI KAMA HUYU, NIMEZOEA KUZINGULIWA SITAKI TENA MAHUSIANO? NI SHETANI”

Soma na hizi

Tupia Comments