Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

AyoTV

Maamuzi ya kwanza ya Bodi ya Ligi kuhusu Yondani kumtemea mate Kwasi

on

Jumapili ya April 29 2018 mchezo wa watani wa jadi kati ya Simba na Yanga ulichezwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam na kuhudhuriwa  na mashabiki mbalimbali, dakika 90 za mchezo huo zilimalizika kwa Simba kupata ushindi wa goli 1-0 lilifungwa na Erasto  Nyoni dakika ya 38, mchezo huo ulikuwa na presha na matukio mbalimbali yalijitokeza.

Moja kati ya tukio lililojitokeza ni tukio la beki wa Yanga Kelvin Yondani kumtemea mate Asante Kwasi wa Simba wakati wa mchezo huo, afisa mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi leo ametangaza maamuzi ya kwanza kuwa wao wameamu kumsimamisha Yondani kucheza hadi suala lake litakapotewa maamuzi na kamati ya nidhamu.

Mrisho Ngassa kuhusu Yondani kumtemea mate Kwasi

Soma na hizi

Tupia Comments