Michezo

Kiasi cha pesa alichotumia Ronaldo kuwanunulia wachezaji wenzie zawadi ya saa za gharama

on

IMG_9857.JPG

Baada ya kuwa na msimu wa mafanikio akishinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia, akiiongoza Real Madrid kutwaa ubingwa wa Copa Del Rey pamoja na Champions League. Hatimaye Cristiano Ronaldo ameamua kuwatunza wachezaji wenzie wa Madrid.

Ronaldo ambaye anapewa nafasi kubwa ya kuwa mchezaji bora wa dunia kwa mara nyingine mwezi ujao, amewanunulia zawadi ya saa zilizotengenezwa maalum kwa ajili yake wachezaji wenzie wote wa Real Madrid.

Cristiano Ronaldo amewanunulia wenzie saa aina ya Bulgari ambazo zimewekwa majina yao na zina thamani ya £6,500 kwa kila saa.

Mchezaji wa kwanza kuonyesha zawadi aliyopewa na Ronaldo ni Alvaro Arbeloa ambaye alipost picha akiwa na saa yake kwenye mtandao wa instagram.

IMG_9797.PNG

Tupia Comments