Tangaza Hapa Ad

Mix

Utafiti wadai mtu mmoja kati ya wanne ni kichaa, Wizara yaeleza sababu

on

Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipata huko.

Moja kati habari zilizoandikwa kwenye magazeti ya Tanzania ni hii ya kutoka gazeti la Jambo Leo yenye kichwa acha habari ‘Watanzania wengi ni vichaa, kila mmoja kati ya wanne ana tatizo hilo’

Gazeti la Jambo leo limeripoti kuwa Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, watoto na wazee, Ummy Mwalimu amesema utafiti unaonesha kuwa kwa kila watu wanne duniani , mmoja ana matatizo ya afya ya akili.

Kwa mujibu wa Waziri Ummy wananchi wanapaswa kuwa makini kuchunguza afya zao za akili  kwa sababu utafiti wa shirika la afya duniani ‘WHO’ zinaashiria kuwa jamii kwa sasa inakumbwa na maradhi mengi ya namna hiyo, Waziri Ummy alibainisha 

>>>’Miongoni mwa watu wanaopata matatatizo ya kiakili ni wachache  tu ambao wanaweza kufikia na kupata huduma ya afya ya akili, hata hao wanohudhuria vituo vya afya, ni wachache wamekuwa wakipata huduma stahiki’

Alifafanua sababu za kijamii zinazoweza kusababisha mtu kupata magonjwa ya akili ni umaskini uliokithiri, kutengwa na kubaguliwa na jamii. sababu nyingine alizitaja kuwa ni kunyanyaswa kimwili na kingono, kuwa tegemezi, kupoteza mali, kazi, ulevi, kukosa huduma muhimu na unyanyapaa.

Source: Jambo Leo

Unaweza kupitia habari zingine kubwa kutoka kwenye magazeti ya Tanzania leo

ULIKOSA HII YA WAZIRI WA AFYA KUTAJA SABABU ZA KUNUNUA DAWA INDIA NA SI KENYA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement