Tangaza Hapa Ad

Michezo

Simba timu ya kwanza kutoka na ushindi dhidi ya Stand United Kambarage

on

Ligi Kuu soka Tanzania bara msimu wa 2016/2017 umeendelea kwa michezo sita kupigwa katika viwanja mbalimbali Tanzania, wakati Mabingwa watetezi Yanga wakiwa Mbeya kucheza dhidi ya Mbeya City, watani zao Simba walikuwa Shinyanga kuwakabili Stand United.

img_4385

Simba wakiwa katika uwanja wa ugenini wenye rekodi nzuri kwa wenyeji Stand United kutokupoteza mchezo katika uwanja huo kwa msimu huu, wamekuwa timu ya kwanza kuondoka na point tatu dhidi ya Stand United katika uwanja wa Kambarage.

img_4349

Katika mchezo huo ambao Simba walikuwa na tahadhari kutokana na Stand United kuwafunga Yanga na Azam FC katika uwanja huo, Simba wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0, goli ambalo lilifungwa na Shiza Kichuya kwa mkwaju wa penati dakika ya 33 baada ya Laudit Mavugo kufanyiwa faulo katika eneo la hatari.

img_4399

ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement