Tangaza Hapa Ad

Mix

NMB na droo ya mwisho ya Ki-college plus.

on

DSC_0519
Oktoba 12 2013 NMB ilizindua promosheni ya Ki-COLLEGE Plus na NMB inayowawezesha wanafunzi wa elimu ya juu wenye akaunti na NMB Student Account.

Pia kupata nafasi ya kuingia kwenye droo na kujishindia zawadi mbalimbali kama simu za mkononi ainaya ‘Samsung Galaxy Pocket Plus 3g’ na kujishindia fulana za NMB.

Zaidi ya  washindi 400 waliofungua NMB Student Account na walioweka amana katika akaunti zao au kujiunga na NMB mobile wameweza kuingia kwenye droo na wamepata nafasi ya kujishindia zawadi kwenye promosheni ya Ki-COLLEGE Plus iliyodumu kwa miezi mitatu.

Katika droo ya mwisho iliyochezwa jana jumla ya washindi 40 wamepata bahati ya kujishindia simu za mkononi aina ya ‘Samsung Galaxy Pocket Plus 3g’ na washindi wengine 100 kujishindia fulana za NMB.

DSC_0514

DSC_0502Mkuu wa kitengo cha Biashara NMB (tatu kushoto) Filbert Mponzi akibonyeza kitufe ili kuwapata washindi wa droo ya mwisho ya Ki-COLLEGE Plus na NMB ambapo washindi 140 wamejishindia zawadi mbalimbali kama vile simu ya mkononi ainaya ‘Samsung Galaxy Pocket Plus 3g’ na kujishindia fulanaza NMB.

Kwanza kushoto ni Meneja Masoko wa NMB, Yusuf Shenyagwa , Menejawa Amana za Watejawa NMB, Boma Raballa,  Meneja Huduma kampuni ya Selcom, Everline Simpilu selcom  na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, MrishoMillao .

 

Tupia Comments

Advertisement