Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

“Mimi ni staa mkali kuliko nyinyi wote” – Tekno Miles

on

Staa mwimbaji Tekno Miles kutoka Nigeria huenda akaingia kwenye matatizo na wasanii wengine baada jana kupost video akisema yeye ni msanii mkali kuliko msanii yeyote barani Afrika kwasa, kitendo hicho kimefanya mashabiki kumjibu kwa matusi na kupelekea staa huyo kuifuta video ndani ya dakika chache.

Hii inakuja siku chache baada ya Billboard kumtaja Tekno kwenye Top 10 ya wasanii wakuwaangalia zaidi mwaka  2017, kitu kinachotafsiriwa kama kimempa jeuri ya kuzungumza chochote ikiwa ni msanii pekee kutoka Afrika kutajwa kwenye list hiyo. 

Kupitia Instagram yake, mwimbaji wa hit single ya Pana ambayo imetazamwa zaidi ya mara milioni 15 Youtube  alindika maneno ya kuonesha hakuna msanii mwingine anayemuhofia kwasasa: “Natengeneza moto ??????. mimi ni zaidi ya yeyote, Mfalme wa muziki wangu #pandajuu #Ushindi.” – Tekno

VIDEO: Ulipitwa na hii performance ya Tekno, Juma Nature, Ommy Dimpoz na Seyi Shay Live kwenye stage ya FIESTA2016? Itazame video hii.

Unazitaka Breaking NEWS na Stori zote? ungana na Millard Ayo kwenye Facebook Twitter Instagram na Youtube na atakuletea matukio yote ya picha, video na habari iwe usiku au mchana…. bonyeza hapa >>> FB Twitter Instagram YouTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement