Tangaza Hapa Ad

Magazeti

TOP NEWS: Zipo hapa kubwa zote kutoka magazeti ya leo Dec 29, 2016

on

Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimekuwekea hapa habari kubwa za leo kutoka kwenye magazeti ya Tanzania, waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.

BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), imesema kuanzia Januari mwakani itaanza kudai fedha za mikopo kwa kupita nyumba kwa nyumba, hasa muda wa usiku.

Mbali na hilo, HESLB wamesema kuwa wapo kwenye mpango wa kuzungumza na washereheshaji wa sherehe (ma-MC), hasa harusi na viongozi wa nyumba za ibada ili waweze kutumia maeneo yao kuwakumbusha wadaiwa hao walipe madeni yao.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo, Abdul-Razaq Badru, alisema kuwa sasa ni wakati mwafaka kuhakikisha madeni yote yanalipwa kwa kutumia kila aina ya njia.

Aliwataka walionufaika na mikopo hiyo kuanza kujisalimisha wenyewe kulipa madeni yao kuepuka kusakwa majumbani na katika nyumba za ibada.

“Tumefanya jitihada mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuandaa mpango wa kuwashirikisha washereheshaji katika shughuli mbalimbali pamoja na nyumba za ibada ili waweze kuwakumbusha wadaiwa wa bodi kurejesha mikopo na ifikapo Januari Mosi, mwakani majina na sura za wadaiwa sugu tutazichapisha gazetini.

“Si hilo tu, pia tutapita nyumba kwa nyumba nchi nzima, hasa muda wa jua linapozama ili kuweza kuwafikia wadaiwa wote ambao walipata mikopo kupitia Bodi ya Mikopo. Mkopo si zawadi ni lazima ulipwe, Walipe ili na wengine waweze kunufaika na fursa ya mikopo. Na wale ambao watakaidi tutawafikisha mahakamani ambako watalipa gharama za uendeshaji wa kesi pamoja na deni wanalodaiwa,” –Badru

Mkurugenzi huyo alisema hivi sasa wameanza utekelezaji wa marekebisho ya Sheria ya Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu, ambapo kwa sasa wanufaika wa mkopo watalazimika kukatwa asilimia 15 badala ya asilimia nane ya awali.

Badru alisema sheria hiyo mpya imeipa meno bodi hiyo pia kuwawajibisha na kuwafikisha mahakamani waajiri endapo watashindwa kukata makato kwa waajiriwa wao ambao ni wanufaika wa mikopo au kuchelewesha kuwasilisha fedha za makato hayo.

“Kwa mabadiliko haya ya sheria, mwajiri sasa ana wajibu wa kuwasilisha majina, kukata na kuwasilisha makato stahiki kutoka katika mishahara ghafi ya waajiriwa wake walionufaika na mikopo ya elimu ya juu,” alisema Badru.

Alisema kwa waajiri ambao hawatawajibika, watalipa faini isiyopungua makato hayo au kifungo cha miezi 36.

Badru alisema pia wametoa siku 14 kuhakikisha kila mwajiri anapitia kumbukumbu zake na kuangalia kiasi walichokata na kuwasilisha katika bodi hiyo kabla timu iliyoundwa kufuatilia madeni hayo haijaanza kufanya kazi.

Alitoa wito kwa waajiri na waajiriwa kuhakikisha wanakusanya kumbukumbu muhimu ili kuepusha usumbufu endapo wataajiri wadaiwa sugu wa bodi hiyo na wakakwepa kutoa taarifa zao mapema.

Alisema kuhusu wanufaika ambao hawapo kwenye mfumo rasmi na mikopo yao imeiva, watalazimika kulipa Sh 100,000 au asilimia 10 ya kipato kinachotozwa kodi kwa mwezi.

“Sheria hii imepita mikononi mwa wadau ambao wamejaribu kupunguza ukali wa maisha, ambapo kwa wanufaika ambao hawako kwenye mfumo rasmi watalazimika kulipa deni lao baada ya miaka miwili badala ya mmoja wa sasa na kwa wale ambao wana ajira wataanza kulipa mara baada ya kuajiriwa,” alisema Badru.

Sambamba na hilo, bodi hiyo imesema hadi sasa  imefanikiwa kukusanya Sh bilioni 140 kutoka kwa wanufaika wa mikopo iliyoiva. Awali deni lilikuwa ni Sh bilioni 300.

Mkurugenzi huyo alisema kiwango cha makusanyo ya mikopo ambayo awali yalikuwa ni Sh bilioni 2 kwa mwezi, hadi kufikia Novemba, mwaka huu yameongezeka na kufikia Sh bilioni 8 kwa mwezi.

Pia wadaiwa sugu waliojitokeza kulipa au kupunguza madeni yao wamefikia 42,700 kati ya 100,000 waliokuwa wanadaiwa awali.

“Katika kuhakikisha waajiri wanakusanya makato yetu, tumekutana na waajiri zaidi ya 10 na kuzungumza nao, ambao wengi wao walikuwa hawafahamu wajibu wao,” alisema Badru.

Kwa upande wa mwanasheria wa bodi hiyo, Luhano Lupogo, alisema mwajiri ana wajibu wa kupeleka makato ya mwajiriwa wake kwa bodi ndani ya siku 15, vinginevyo atalipa faini isiyopungua makato au kifungo cha miaka mitatu jela.

Alisema sheria hiyo ya mwaka 2004, namba 21 (2) imeanza kutumika Novemba 18, mwaka huu ambapo pia mwajiri ana wajibu wa kuwasilisha katika bodi orodha ya waajiriwa wake ambao ni wahitimu wa Stashahada au Shahada.

VIDEO: AYO TV MAGAZETI: Mapya yaibuka nyoka wa maajabu, hamna aliyelia Msibani, Bonyeza video hapa chini kutazama.

Unazitaka Breaking NEWS na Stori zote? ungana na Millard Ayo kwenye Facebook Twitter Instagram na Youtube na atakuletea matukio yote ya picha, video na habari iwe usiku au mchana…. bonyeza hapa >>> FB Twitter Instagram YouTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement