Tangaza Hapa Ad

Mix

Jeshi la Polisi limetangaza magari mapya yaliyoruhusiwa kubeba abiria

on

Kutokana na mahitaji ya usafiri katika kipindi kuelekea mwisho wa mwaka 2016 pamoja na msimu wa sikukuu, Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani na pamoja na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchikavu na Majini, SUMATRA limetangaza kutoa vibali kwa mabasi aina ya Eicher na Coaster ili kufanya safari za mikoani.

Aidha kupitia taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi, Kikosi cha usalama barabarani Mohammed Mpinga pia amesema kuwa jeshi hilo limesitisha utendaji wa chama cha kutetea abiria ‘CHAKUA’ mikoani kutokana na kukiuka maadili na kuanzia sasa watabaki na watendaji wa kituo cha mabasi Ubungo pekee.

“Tumeamua kutoa vibali kwenye mabasi mengine ili kurahisisha usafiri kutokana na kuanza kuongezeka kwa abiria, mfano juzi kwenye kituo cha Ubungo yalitoka mabasi 421, jana yametoka mabasi 470 sasa tumeamua kuongeza na Coaster na tumeshafanya ukaguzi mabasi yote yako salama” – Kamanda Mpinga

Taarifa kamili nimekuwekea kwenye video hii, Bonyeza play kutazama.

VIDEO: Kuelekeza Sikukuu za mwisho wa mwaka, Jeshi la Polisi limetoa agizo kwa wananchi kuhusu usalama. Tazama video hii.

Unazitaka Breaking NEWS na Stori zote? ungana na Millard Ayo kwenye Facebook Twitter Instagram na Youtube na atakuletea matukio yote ya picha, video na habari iwe usiku au mchana…. bonyeza hapa >>> FB Twitter Instagram YouTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement